-
MaandaliziDakika 30
-
KupikaDakika 50
-
Walaji4
Biriani ya mboga, ni chakula kitamu na chenye harufu nzuri ambacho hupikwa kwa kutumia wali mweupe uliopikwa, maziwa, mboga mchanganyiko, mtindi, njugu mchanganyiko, pamoja na viungo. Biriani hii ya mboga kama zilizvyo biriani nyingine zote, ni chakula ambacho chafaa kuliwa kwenye sherehe au sikukuu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biriani hii ya mboga.
Ingredients
Directions
Chukua kikombe chenye maziwa, kisha roweka zafarani ndani ya hicho kikombe chenye maziwa kwa muda wa dakika 30.
Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mchanganyiko wa njugu kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo ona zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia, kisha epua na uweke pembeni.
Chukua sufuria kubwa lenye siagi na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha siagi iyeyuke. Weka kwenye hilo sufuria, mdalasini, karafuu, iliki, pamoja na majani ya mbei, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Weka vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona vitunguu maji vimeiva.
Weka tangawizi pamoja na vitunguu swaumu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.
Weka mchanganyiko wa mboga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7.
Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga, halafu acha ichemke kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona mtindi umekaribia kukauka, kisha epua na uweke pembeni.
Washa jiko la kuoka na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto.
Chukua sufuria jingine kubwa. Mimina mchuzi wa mboga mchanganyiko uliyoipika kwenye hilo sufuria.
Weka nusu ya wali mweupe uliopikwa juu ya huo mchuzi, kisha sambaza vizuri.
Weka mchanganyiko wa mboga ulioupika juu ya huo wali, kisha sambaza vizuri.
Nyunzia limao, majani ya giligilani, pamoja na majani ya minti, juu ya huo mchanganyiko wa mboga.
Weka nusu ya wali uliobaki, kisha sambaza vizuri.
Nyunyizia maziwa yenye zafarani juu ya huo wali, kisha funika vizuri sufuria hilo kwa kutumia aluminium foil.
Weka sufuria hilo ndani ya jiko la kuoka, kisha oka kwa muda wa dakika 30, au hadi utakapo ona biriani imeiva. Ondoa sufuria hilo kwenye jiko la kuoka na uliweke pembeni.
Weka mchanganyiko wa njugu ulizo zikaanga kwenye hilo sufuria lenye biriani, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review