-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 10
-
Walaji4
Biringanya za kuponda zenye haradali, ni mboga tamu ambayo hupikwa kwa kutumia biringanya zilizopondwa, choroko, limao, pamoja na viungo vya aina mbalimbali kama vile haradali. Mboga hii yafaa kula pamoja na chapati, wali au mkate. Fuata hatua zifuatazo, ili ukifunze jinsi ya kupika biringanya za kuponda zenye haradali.
Ingredients
Directions
Chukua kontena. Weka biringanya ndani ya hilo kontena, halafu funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye jiko la microwave na upike katika moto mkubwa kwa muda wa dakika 5 mpaka 6, au hadi utakapo ona biringanga zimeiva. Ondoa kontena hilo kwenye jiko la microwave na uliweke pembeni ili biringanya zipoe, kisha ziponde vizuri.
Weka ndani ya hilo kontena, majani ya giligilani, chumvi, pamoja na limao, kisha changanya vizuri.
Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka choroko kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30.
Weka mbegu za haradali pamoja na majani ya mvuje, kisha koroga vizuri. Epua mchanganyiko huu na umimine kwenye kontena lenye mchanganyiko wa biringanya, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.
Leave a Review