Jarida la Mapishi

Biringanya za kuponda zenye viazi

Biringanya za kuponda zenye viazi | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 35
  • Walaji
    4

Biringanya za kuponda zenye viazi, mboga tamu na rahisi kupika, ambayo hupikwa kwa kutumia biringanya zilizopondwa, nyanya, viazi mviringo, pamoja na viungo. Mboga hii yafaa kula pamoja na chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biringanya hizi za kuponda zenye viazi.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena. Weka biringanya ndani ya hilo kontena, halafu funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye jiko la microwave na upike katika moto mkubwa kwa muda wa dakika 5 mpaka 6, au hadi utakapo ona biringanga zimeiva. Ondoa kontena hilo kwenye jiko la microwave na uliweke pembeni ili biringanya zipoe, kisha ziponde vizuri.

    Step2

    Chukua sufuria dogo lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, tangawizi, mbegu za giligilani, viazi mviringo, nyanya, majani ya giligilani, pamoja na chumvi, halafu funika sufuria, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.

    Step3

    Punguza moto na uweke moto mdogo. Weka biringanya ulizo ziponda, halafu pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 15 mpaka 20, au hadi utakapo ona viazi vimeiva, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.