Jarida la Mapishi

Biringanya zenye giligilani

Biringanya zenye giligilani | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 15
  • Walaji
    4

Biringanya zenye giligilani, ni mboga tamu ambayo hupikwa kwa kutumia biringanya pamoja na viungo vya aina mbalimbali, kama vile majani ya giligilani. Mboga hii yafaa kula pamoja na wali au chapati. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biringanya hizi zenye giligilani.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena. Weka biringanya ndani ya hilo kontena, halafu funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye jiko la microwave na upike katika moto mkubwa kwa muda wa dakika 4, au hadi utakapo ona biringanga zimeiva. Ondoa kontena hilo kwenye jiko la microwave na uliweke pembeni.

    Step2

    Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, binzari nyembamba, mbegu za haradali, mbegu za uwatu, vitunguu swaumu, majani ya mvuje, mbegu za giligilani, majani ya minti, pamoja na binzari ya manjano, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kaa muda wa sekunde 30.

    Step3

    Weka biringanya pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.

    Step4

    Weka majani ya giligilani halafu funika kikaango, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona biringanya zimekuwa laini.

    Step5

    Weka mango powder halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.