-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 45
-
Walaji4
Biringanya zenye nazi, ni mboga tamu iliyo sheheni ladha ya nazi, ambayo hupikwa kwa kutumia biringanya, nazi, kitunguu maji, majani ya minti, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mboga hii yafaa sana kupika katika msimu wa kiangazi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biringanya hizi zenye nazi.
Ingredients
Directions
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, nazi iliyokunwa, tangawizi, vitunguu swaumu, pamoja na vitunguu maji, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Weka mbegu za giligilani, garam masala, pamoja na binzari ya manjano, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka mchanganyiko wa nazi ulio usaga kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, au hadi utakapo ona mchanganyiko huo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka biringanya, tui la nazi, pamoja na chumvi halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke kwa muda wa dakika 4.
Punguza moto na uweke moto wa wastani, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 20 mpaka 30, au hadi utakapo ona biringanya zimeiva na kuwa laini.
Weka limao, majani ya giligilani, pamoja na majani ya minti halafu koroga vizuri, kisha acha ichemke kwa muda wa dakika 2 mpaka 4.
Nyunyizia garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review