Jarida la Mapishi

Biringanya zenye ufuta

Biringanya zenye ufuta | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 15
  • Walaji
    4

Biringanya zenye ufuta, ni mboga yenye ladha nzuri na rahisi kupika, ambayo hupikwa kwa kutumia biringanya, mbegu za ufuta, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Mboga hii yafaa kula pamoja na wali au tambi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupoka kitoweo hiki cha biringanya zenye ufuta.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikaango kidogo na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mbegu za ufuta kwenye hicho kikaango, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step2

    Chukua kinu. Weka ndani ya hicho kinu mbegu za ufuta ulizo zikaanga, kisha twanga hadi utakapo ona mbegu hizo zimesagika vizuri.

    Step3

    Chukua kikaango cha ukubwa wa wastani na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka kwenye hicho kikaango, biringanya pamoja na chumvi, halafu funika kikaango, kisha pika kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa biringanya hizo kwenye kikaango na uziweke pembeni kwenye kontena, kisha funika vizuri kontena hilo. Kumbuka kuzigeuza mara 1 au 2 wakati unapika.

    Step4

    Weka olive oil kwenye kikaango hicho hicho, kisha acha mafuta yapate moto. Weka binzari nyembamba, vitunguu swaumu, majani ya giligilani, biringanya ulizo zipika, pamoja na mango powder, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.

    Step5

    Nyunyizia garam masala pamoja na mbegu za ufuta, halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.