-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 25
-
Walaji4
Biringanya zenye ukwaju, ni mboga tamu yenye viungo, iliyo sheheni ladha ya utamu na uchachu, ambao unatokana na ukwaju unaowekwa katika pishi hili. Mboga hii yafaa kula pamoja na wali mweupe. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biringanya hizi zenye ukwaju.
Ingredients
Directions
Chukua kikaango kikubwa. Weka biringanya kwenye hicho kikaango, kisha funika kikaango. Weka kikaango kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha pika biringanya hizo huku ukizigeuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, au hadi utakapo ona zimeanza kubadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Nyunyizia olive oil juu ya hizo biringanya.
Weka vitunguu swaumu, mbegu za giligilani, Chaat Masala, pamoja na chumvi, halafu funika kikaango, kisha pika mchanganyiko huo huku ukizigeuza biringanya mara kwa mara kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona biringanya zimeiva na kuwa laini.
Weka majani ya giligilani pamoja na Tamarind Paste, halafu pika mchanganyiko huo huku ukizigeuza biringanya mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review