Jarida la Mapishi

Biringanya zenye utamu na uchachu

  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 30
  • Walaji
    4

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mdalasini, binzari nyembamba, pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.

    Step2

    Weka vitunguu swaumu halafu kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa sekunde 30, kisha epua na uweke pembeni kwenye kontena.

    Step3

    Weka biringanya kwenye sufuria hilo hilo, halafu weka moto mkubwa, kisha acha zipate moto.

    Step4

    Ukiona zimepata moto, punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu funika sufuria, kisha pika biringanya hizo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona biringanya zimeanza kuiva.

    Step5

    Weka mchanganyiko wa vitunguu maji ulio ukaanga, mbegu za giligilani, pamoja na chumvi, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona biringanya zimeiva na kuwa laini.

    Step6

    Weka Tamarind Paste pamoja na sukari, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step7

    Weka majani ya giligilani, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2 mpaka 3.

    Step8

    Nyunyizia garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.