Jarida la Mapishi

Biringanya zenye vitunguu swaumu

Biringanya zenye vitunguu swaumu | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 20
  • Walaji
    4

Biringanya zenye vitunguu swaumu, ni mboga tamu ambayo hupikwa kwa kutumia biringanya, vitunguu maji, nyanya, pamoja na viungo vya aina mbalimbali kama vile vitunguu swaumu. Mboga hii yafaa kula pamoja na chapati au wali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biringanya hizi zenye vitunguu swaumu.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena. Weka biringanya ndani ya hilo kontena, halafu funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye jiko la microwave na upike katika moto mkubwa kwa muda wa dakika 4, au hadi utakapo ona biringanga zimeiva. Ondoa kontena hilo kwenye jiko la microwave na uliweke pembeni.

    Step2

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, binzari nyembamba, pilipili manga, vitunguu maji, pamoja na vitunguu swaumu, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, au hadi utakapo ona vitunguu vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step3

    Weka nyanya, mbegu za giligilani, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1.

    Step4

    Weka biringanya pamoja na majani ya giligilani, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona biringanya zimekuwa laini.

    Step5

    Nyunyizia garam masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.