-
MaandaliziDakika 20
-
Kupika-
-
Walaji4
Bisi za chocolate, ni kitafunio kilicho sheheni ladha nzuri ya chocolate, ambazo hupikwa kwa kutumia cocoa powder, sukari, pamoja na mdalasini. Bisi hizi zafaa kula kama kitafunio cha kawaida katika muda na wakati wowote ule. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika bisi hizi za chocolate.
Ingredients
Directions
Step1
Chukua bakuli kubwa. Weka bisi zilizopikwa ndani ya hilo bakuli, kisha weka pembeni.
Step2
Chukua bakuli ndogo. Weka ndani ya hilo bakuli, mafuta ya nazi, sukari, cocoa powder, pamoja na mdalasini, kisha changanya vizuri mchanganyiko huo kwa kuupiga piga.
Step3
Chukua mchanganyiko wa bakuli ndogo na umimine kwenye bakuli kubwa lenye bisi, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.
Leave a Review