-
MaandaliziDakika 5
-
KupikaDakika 5
-
Walaji4
Bisi za limao na viungo, ni bisi zilizo sheheni ladha ya kipekee ya uchachu pamoja na harufu nzuri ya limao na viungo. Bisi hizi zafaa kula kama kitafunio cha kawaida hasa wakati ambao unatizama filamu. Pia waweza kuandaa bisi hizi kwa ajili ya hafla au sherehe. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika bisi hizi za limao na viungo.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha achs sufuria lipate moto. Weka mbegu za binzari nyembamba kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1 mpaka 2. Epua mbegu hizo za binzari nyembamba na uziweke pembeni kwenye bakuli safi.
Weka kwenye hilo hilo sufuria olive oil pamoja na mahindi ya bisi, halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria. Pika bisi hizo huku ukitikisa sufuria mara kwa muda wa dakika 3, au hadi utakapo sikia bisi zimeanza kupasuka. Endelea kutikisa sufuria wakati bisi zinaendelea kupasuka, ili kuzuia bisi zisiungue.
Ukiona bisi zote zimepasuka, epua na uziweke pembeni kwenye bakuli kubwa.
Weka kwenye hilo bakuli lenye bisi, curry powder, mdalasini, maganda ya limao yaliyo kunwa, (grated), binzari nyembamba ulizo zikaanga, pamoja chumvi, kisha changanya vizuri, halafu acha zipoe kwa ajili ya kula.
Leave a Review