-
MaandaliziSaa 1 Dk. 15
-
KupikaDakika 15
-
Walaji25
Biskuti za aprikoti na nazi, ni biskuti tamu, rahisi kupika na zenye ladha ya matunda halisi ya aprikoti pamoja na nazi. Biskuti hizi zafaa zaidi kuliwa kwenye sherehe. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biskuti hizi za aprikoti na nazi.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, unga wa ngano, nazi, shayiri, matunda ya aprikoti, chumvi, pamoja na baking soda, kisha changanya vizuri.
Chukua bakuli nyingine ndogo. Weka ndani ya hiyo bakuli, siagi, light brown sugar, sukari na vanilla extract, halafu changanya vizuri.
Chukua mchanganyiko wa bakuli ndogo ya pili, na umimine kwenye mchanganyiko wa bakuli la kwanza. Weka dark chocolate chips, kwenye hilo bakuli la kwanza, kisha changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.
Leave a Review