-
MaandaliziSaa 1
-
KupikaDakika 15
-
Walaji30
Biskuti za chocolate, ni biskuti ambazo ni rahisi sana kupika. Biskuti hizi zinapikwa kwa kutumia nutella, unga wa cocoa, pamoja na dark chocolate chips. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza biskuti hizi za chocolate.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi, light brown sugar, pamoja na sukari, kisha changanya vizuri.
Weka nutella, vanilla extract, mayai na uchanganye vizuri, halafu weka unga wa ngano, cocoa powder, chumvi, baking soda na dark chocolate chips, kisha changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.
Leave a Review