-
MaandaliziSaa 1 Dk. 15
-
KupikaDakika 15
-
Walaji30
Biskuti za chumvi na chocolate, ni biskuti tamu na rahisi kupika zenye ladha ya chocolate yenye chumvi chumvi. Biskuti hizi zafaa kula kama kitafunio cha kawaida wakati wowote. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biskuti hizi za chumvi na chocolate.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, dark chocolate chips pamoja na sukari, kisha weka bakuli hilo ndani ya sufuria lenye maji ya moto, halafu acha viyeyuke. Ukiona vimesha yeyuka, weka mafuta ya nazi, kisha changanya vizuri.
Weka light brown sugar, dark brown sugar na mayai, halafu endelea kuchanganya.
Weka unga wa ngano, cocoa powder, chumvi, pamoja na baking powder, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 15, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.
Leave a Review