-
MaandaliziDakika 45
-
KupikaDakika 15
-
Walaji20
Biskuti za karanga na chocolate, ni biskuti tamu na laini zilizo sheheni ladha ya karanga na chocolate. Biskuti hizi ni rahisi sana kupika na unaweza kuzipika katika muda mfupi sana wa ndani ya saa 1 tu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biskuti hizi za karanga na chocolate.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi pamoja na sukari, kisha changanya vizuri.
Weka yai na uchanganye vizuri, halafu weka unga wa ngano, baking soda, baking powder, chumvi, pamoja na dark chocolate chips, kisha changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 12 mpaka 15, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.
Leave a Review