-
MaandaliziSaa 1
-
KupikaDakika 15
-
Walaji30
Biskuti za karanga, ni biskuti tamu ambazo zinaweza kuliwa muda wowote kama kitafunio cha kawaida. Biskuti hizi hupikwa kwa kutumia siagi, siagi ya karanga pamoja na karanga mbichi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biskuti hizi za karanga
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi pamoja na siagi ya karanga, kisha changanya vizuri. Weka light brown sugar na uendelee kuchanganya kwa muda wa dakika 5 zaidi.
Weka yai na uchanganye vizuri, halafu weka unga wa ngano, baking powder, chumvi na karanga, kisha changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.
Leave a Review