-
MaandaliziSaa 1
-
KupikaDakika 15
-
Walaji20
Biskuti za pasheni na machungwa, ni biskuti zenye ladha ya utamu na uchachu ambao unatokana na mchanganyiko wa matunda ya pasheni na machungwa. Biskuti hizi zafaa kula kama kitafunio cha kawaida pamoja na juisi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika biskuti hizi za pasheni na machungwa.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi, sukari, pamoja na vanilla extract, kisha changanya vizuri.
Weka yai, maganda ya chungwa na juisi ya pasheni, halafu endelea kuchanganya.
Weka unga wa ngano, chumvi, pamoja na baking powder, kisha changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.
Leave a Review