-
MaandaliziSaa 1
-
KupikaDakika 15
-
Walaji30
Biskuti za pilipili na chocolate, ni biskuti zenye ladha kali ya pilipili. Biskuti hizi hupikwa kwa kukutumia unga wa ngano, pilipili nyekundu, chocolate, pamoja na mdalasini. Hakikisha una glasi ya maziwa pembeni wakati unakula biskuti hizi kwa sababu pilipili iliyomo ndani ya biskuti hizi ni kali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza biskuti hizi za pilipili na chocolate.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi, sukari, pamoja na dark brown sugar, kisha changanya vizuri.
Weka mayai, vanilla extract na uchanganye vizuri, halafu weka unga wa ngano, cocoa powder, chumvi, pilipili ya unga, baking powder, pamoja na dark chocolate chips, kisha changanya vizuri kwa kutumia mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sinia la kuoka biskuti (cookie/biscuit sheet), na uweke ndani ya hilo sinia karatasi ya kuokea (baking paper). Weka vijiko vya mchanganyiko wa biskuti, kwenye hilo sinia la kuoka biskuti, hadi mchanyiko wote wa biskuti utakapo malizika.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sinia la kuoka biskuti ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 10 mpaka 15, au hadi utakapo ona biskuti zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Biskuti zikisha iva, zitoe kwenye jiko la kuoka na uziweke pembeni ili zipoe kabla ya kula.
Leave a Review