-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 5
-
Walaji2
Chai ya kijani, ni chai ang'avu na yenye ladha nyepesi. Chai hii ya kijani ni moja ya chai nzuri sana hasa kutokana na ladha yake tamu pamoja na faida zake kiafya. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika chai hii ya kijani.
Ingredients
Directions
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, punje 2 za lozi pamoja na mbegu za iliki, kisha saga vizuri hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huu kwenye mashine ya kusaga, kisha weka kwenye kontena.
Weka mdalasini kwenye hilo kontena, halafu changanya vizuri, kisha weka pembeni.
Weka punje 4 za lozi zilizobaki kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, kisha saga hadi utakapo ona lozi hizo zimesagika vizuri na kuwa laini.
Chukua sufuria dogo. Weka kwenye hilo sufuria, maji, majani ya chai, sukari, pamoja na mchanganyiko wa lozi uliomo kwenye kontena, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 2, kisha epua na uweke pembeni.
Chukua vikombe 2 pamoja na chujio. Weka nusu ya lozi ulizo zisaga kwenye kikombe cha kwanza, na nusu ya lozi iliyobaki kwenye kikombe cha pili.
Chuja chai ndani ya hivyo vikombe. Ongeza sukari kadiri ya mahitaji yako, kisha koroga vizuri, tayari kwa kunywa.
Leave a Review