-
MaandaliziSaa 1 Dk. 5
-
KupikaDakika 25
-
Walaji12
Cupcakes za balungi, ni cupcakes tamu zinazopikwa kwa kutumia matunda halisi ya balungi pamoja na maganda yake yaliyokunwa. Cupcakes hizi zafaa sana kula katika msimu wa masika au kwenye sherehe ya aina yoyote ile. Fuata hatua zifuatazo ili ujifunze jinsi ya kutengeneza cupcakes hizi za balungi.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi, pamoja na sukari, kisha changanya vizuri.
Weka maganda ya balungi na mayai, halafu endelea kuchanganya.
Weka unga wa ngano, chumvi, baking powder, pamoja na buttermilk, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka cupcakes (cupcakes pan) lenye matundu 12 ya cupcakes, na uweke ndani ya hayo matundu karatasi za kuokea cupcake (cupcake papers). Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka cupcakes.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka cupcakes ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 20 mpaka 25, au hadi utakapo ona cupcakes zimeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Cupcakes zikisha iva, ziondoe kwenye jiko la kuoka, kisha ziweke pembeni ili zipoe, zikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka cupcakes. Cupcakes zikishapoa, unaweza kuzitoa ndani ya sufuria la kuoka cupcakes, tayari kwa kula.
Leave a Review