Jarida la Mapishi

Curry powder

Curry powder | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 5
  • Walaji
    1

Curry powder, ni mchanganyiko wa viungo, ambao husiadia kuongeza ladha kwenye chakula. Curry powder yaweza kutumika kwenye chakula cha aina yoyote ile; kama vile supu, mchuzi, saladi, n.k. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza curry powder hii kwa ajili ya kuiuza, au kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikaango cha ukubwa wa wastani chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka vitunguu swaumu kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, au hadi utakapo ona vimeiva.

    Step2

    Weka mbegu za shamari, mbegu za binzari nyembamba, mbegu za uwatu, mbegu za iliki, majani ya mbei, pamoja na zafarani, halafu kaanga huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step3

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga mchanganyiko ulio ukaanga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena.

    Step4

    Weka ndani ya hilo kontena, tangawizi, mdalasini, karafuu, basibasi, pamoja na kungumanga, kisha changanya vizuri.

    Step5

    Weka viungo hivyo kwenye chombo safi chenye mfuniko, kisha hifadhi mahali pakavu penye baridi.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.