Jarida la Mapishi

Garam masala

Garam masala | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 5
  • Walaji
    1

Garam masala, ni mchanganyiko wa viungo, ambao husiadia kuongeza ladha kwenye chakula. Garam masala yaweza kutumika kwenye chakula cha aina yoyote ile; kama vile supu, mchuzi, pilau, n.k. Neno “Garam” lina maana ya moto na Neno “Masala” lina maana ya viungo mchanganyiko. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeza garam masala hii kwa ajili ya kuiuza, au kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kikaango cha ukubwa wa wastani na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka kwenye hicho kikaango, mbegu za shamari, mbegu za binzari nyembamba, mbegu za pilipili manga, mbegu za iliki, pamoja na zafarani, halafu kaanga bila kutumia mafuta huku ukikoroga na kutikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step2

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga mchanganyiko ulio ukaanga, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena.

    Step3

    Weka ndani ya hilo kontena, mdalasini, tangawizi, karafuu, basibasi, pamoja na kungumanga, kisha changanya vizuri.

    Step4

    Rudisha kikaango kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha kikaango kipate moto. Weka mchanganyiko uliomo kwenye kontena kwenye hicho kikaango, halafu kaanga huku ukikoroga mara kwa mara, hadi utakapo ona mchanganyiko huo umepata moto, kisha epua na uweke pembeni ili ipoe.

    Step5

    Weka viungo hivyo kwenye chombo safi chenye mfuniko, kisha hifadhi mahali pakavu penye baridi.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.