-
MaandaliziDakika 30
-
Kupika-
-
Walaji3
Ice cream ya chai, ni ice cream ambayo hutengenezwa kwa kutumia majani ya chai, maziwa, pamoja na krimu. Ice cream hii ni maarufu sana nchini Japan, pia katika nchi za Madhariki mwa bara la Asia. Ice cream hii yafaa kula kama kitindamlo, baada ya mlo wowote ule. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza ice cream hii ya chai.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria ndogo. Weka kwenye hilo sufuria maji pamoja na majani ya chai, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto mkubwa hadi utakapo ona chai imechemka. Epua chai hiyo na uweke pembeni.
Chukua bakuli ndogo. Weka ndani ya hilo bakuli, viini vya mayai pamoja na sukari, kisha changanya vizuri. Mimina mchanganyiko huu kwenye sufuria lenye chai. Mimina maziwa, kisha koroga vizuri.
Chukua sufuria kubwa. Weka maji ya moto kwenye hilo sufuria. Weka mchanganyiko wa chai ndani ya hilo sufuria lenye maji ya moto, kisha changanya kwa kukoroga mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 10.
Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena mchanganyiko wa chai ulio changanya, kisha funika vizuri kontena hilo na uliweke kwenye friji kwa muda wa saa 4.
Baada ya saa 4, ondoa kontena hilo kwenye friji, kisha mimina mchanganyiko huo wa ice cream kwenye mashine ya kutengenezea ice cream (Ice Cream Maker Cooler). Washa mashine hiyo kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona ice cream imekuwa nzito na laini.
Ondoa ice cream hiyo kutoka kwenye mashine ya kutengeneza ice cream, kisha pakua kwenye bakuli safi, tayari kwa kula.
Leave a Review