Jarida la Mapishi

Juisi ya karoti na chungwa

Juisi ya karoti na chungwa | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 10
  • Kupika
    -
  • Walaji
    1

Juisi ya karoti na chungwa, ni juisi yenye afya, safi na rahisi kutengeneza. Juisi hii ina virutubisho vya Vitamini A na C kwa wingi, ambavyo hisaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini, ili mwili uweze kupambana vyema na magonjwa pamoja na maambukizi ya aina mbalimbali. Fuata hatua zifuatazo, ili kujifunza jinsi ya kutengeneza juisi hii ya karoti na chungwa.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, karoti, chungwa, nanasi, maji, pamoja na sukari, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wa juisi umesagika vizuri.

    Step2

    Chuja juisi kwa kutumia chujio, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi kabla ya kunywa.

    Conclusion

    Unaweza kuongeza maji kwenye juisi hii kadiri upendavyo, endapo utaona maji yaliyomo katika juisi hii ni kidogo.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.