-
MaandaliziDakika 35
-
Kupika-
-
Walaji1
Juisi ya zabibu ni juisi safi, ya kuburudisha na yenye virutubisho vingi. Ladha na virutubisho unavyo vipata kwa kuitengeneza mwenyewe juisi hii, ni bora kuliko juisi ya kununua dukani. Kuna njia mbili za kutengeneza juisi hii. Njia ya kwanza ni kwa kuzichemsha zabibu, halafu baadae uzisage ziwe juisi. Njia hii hitumika ili kuifanya juisi ikae mda mrefu zaidi bila kuharibika. Na njia ya pili, ndio hii ya kusaga matunda haya ili yawe juisi, pasipo kuyachemsha. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza juisi hii ya zabibu.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli, weka kijiko 1 cha chakula cha chumvi pamoja na vijiko 2 vya chai vya ndimu, kisha koroga vizuri halafu roweka zabibu hizo ndani ya hayo maji, kwa muda wa dakika 30.
Baada ya dakika 30, mwaga maji uliyotumia kuroweka zabibu, halafu osha zabibu hizo kwenye maji yanayo tiririka. Hatua hii ya kuroweka zabibu, husaidia kuondoa mabaki ya dawa, yaliyo nyunyiziwa kwenye zabibu shambani.
Chukua zabibu na uziweke kwenye mashine ya kusaga pamoja na limao iliyo kamuliwa, maji na sukari, kisha saga hadi utakapo ona juisi imesagika vizuri na kuwa laini.
Chuja juisi kwenye bakuli safi kwa kutumia chujio, kisha imimine kwenye jagi au chupa safi, halafu iweke friji ili ipate baridi kabla ya kunywa.
Conclusion
Unaweza kuongeza maji kwenye juisi hii kadiri upendavyo, endapo utaona maji yaliyomo katika juisi hii kidogo.
Leave a Review