Jarida la Mapishi

Kahawa ya ice cream

Kahawa ya ice cream | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 5
  • Kupika
    -
  • Walaji
    2

Kahawa ya ice cream, ni kinywaji baridi chenye ladha ya kipekee, ambacho hutengenezwa kwa kutumia kahawa, maziwa, pamoja na ice cream ya vanilla. Kahawa hii ni tofauti sana na vinywaji vingine vya kahawa ulivyo vizoea, kwa sababu kahawa hii hunywewa ikiwa ya baridi. Kinywaji hiki cha kahawa chafaa sana kunywa katika msimu wa kiangazi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza kahawa hii ya ice cream.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, maziwa, sukari, kahawa, pamoja na kikombe 1 cha ice cream ya vanilla, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vizuri na kutoa povu.

    Step2

    Chukua glasi mbili ndefu. Weka na ugawe ice cream ya vanilla iliyobaki ndani ya hizo glasi.

    Step3

    Mimina mchanganyiko wa kahawa ulio usaga ndani ya hizo glasi, tayari kwa kunywa.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.