-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 10
-
Walaji2
Kahawa ya viungo, ni kinywaji ambacho hupikwa kwa kuchemsha kahawa pamoja viungo vya aina mbalimbali kama vile, iliki, mdalasini na karafuu. Kahawa hii yafaa kunywa pamoja na kitafunio chochote ukipendacho hasa katika kipindi cha msimu wa sikukuu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza kahawa hii ya viungo.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria. Weka kwenye hilo sufuria, maji, mdalasini, karafuu, pamoja na iliki, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka, hadi utakapo ona maji yamebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Weka kahawa, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, halafu funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 1, kisha epua na uweke pembeni ipoe.
Mimina kahawa kwenye chombo safi, kisha iweke kwenye friji kwa muda wa saa 2 mpaka siku 2.
Chukua vikombe 2 pamoja na chujio. Chuja kahawa ndani ya hivyo vikombe. Mimina maziwa, kisha koroga vizuri, tayari kwa kunywa.
Conclusion
Kahawa hii yafaa kunywa ikiwa ya baridi. Tafadhali, usipashe moto kahawa hii.
Leave a Review