-
MaandaliziDakika 15
-
KupikaDakika 45
-
Walaji10
Keki ya aprikoti, ni keki tamu inayopikwa kwa kutumia matunda halisi ya aprikoti yaliyo katwa katwa na kuondolewa kokwa. Keki hii yafaa kula kama kitindamlo katika msimu wa sikukuu. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya aprikoti.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, mayai, sukari, vanilla extract, pamoja na maganda ya limao, kisha changanya vizuri.
Weka mafuta ya kupikia na sour cream, halafu endelea kuchanganya.
Weka unga wa ngano, baking powder, chumvi, pamoja na matunda ya aprikoti, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 40 mpaka 45, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.
Leave a Review