-
MaandaliziDakika 30
-
KupikaDakika 45
-
Walaji10
Keki ya blackberry na chocolate, ni keki inayopikwa kwa kutumia matunda halisi ya blackberry pamoja na chocolate. Keki hii yafaa kuliwa kama kitindamlo katika hafla ama sherehe ya aina yoyote ile. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya blackberry na chocolate.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, mafuta ya kupikia, pamoja na sukari, kisha changanya vizuri.
Weka mayai na mtindi, halafu endelea kuchanganya.
Weka unga wa ngano, unga wa mahindi, baking powder, chumvi, dark chocolate chips, pamoja na matunda ya blackberry, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 30 mpaka 35, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.
Leave a Review