-
MaandaliziDakika 15
-
KupikaDakika 35
-
Walaji8
Keki ya chocolate, ni mojawapo ya keki zinazopendwa sana. Uzuri wa keki ni kwamba unaweza kuipika kwa kutumia mahitaji ambayo yanapatikana kwa urahisi popote pale ulipo. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya chocolate.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, unga wa ngano, baking powder, chumvi, cocoa powder pamoja na sukari, kisha changanya vizuri.
Chukua bakuli nyingine ndogo. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi, mtindi, mayai, pamoja na vanilla extract, kisha changanya vizuri.
Chukua mchanganyiko wa bakuli ndogo ya pili, na umimine kwenye mchanganyiko wa bakuli la kwanza, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 30 mpaka 35, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.
Recipe Reviews