-
MaandaliziDakika 10
-
KupikaDakika 50
-
Walaji10
Keki ya chocolate na maboga, ni keki tamu iliyo sheheni ladha ya chocolate, ambayo hupikwa kwa kutumia cocoa powder, viungo, pamoja na boga lililo sagwa. Keki hii yafaa sana kuliwa katika sherehe za msimu wa vuli. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya chocolate na maboga.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi pamoja na light brown sugar, kisha changanya vizuri.
Weka mayai, vanilla extract, boga lililo sagwa, sour cream na buttermilk, halafu endelea kuchanganya.
Weka unga wa ngano, cocoa powder, baking powder, baking soda, chumvi, mdalasini, tangawizi, pamoja na star anise, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 10, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 45 mpaka 50, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.
Leave a Review