-
MaandaliziDakika 35
-
KupikaDakika 40
-
Walaji10
Keki ya jozi na ndizi, ni keki iliyo sheheni ladha ya ndizi. Keki hii hupikwa kwa kutumia unga wa ngano, ndizi mbivu zilizo katwa katwa, pamoja na njugu za jozi. Keki hii yafaa kula pamoja na kikombe cha kahawa au chai. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya jozi na ndizi.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, unga wa ngano, jozi, baking soda, chumvi, pamoja na mdalasini, kisha changanya vizuri.
Chukua bakuli nyingine ndogo. Weka ndani ya hiyo bakuli, siagi, light brown sugar na mayai, kisha changanya vizuri. Weka maziwa pamoja na ndizi, halafu endelea kuchanganya.
Chukua mchanganyiko wa bakuli ndogo ya pili, na umimine kwenye mchanganyiko wa bakuli la kwanza, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 10, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 35 mpaka 40, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.
Leave a Review