-
MaandaliziDakika 25
-
KupikaDakika 35
-
Walaji8
Keki ya karanga na ndizi, ni keki isiyokuwa na gluteni inayopikwa kwa kutumia siagi ya karanga pamoja ndizi. Keki hii yafaa sana kuliwa kwenye sherehe au matukio maalum, kama vile, Valentine's Day au Birthday. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya karanga na ndizi.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi ya karanga, siagi, pamoja na sukari, kisha changanya vizuri.
Weka mayai, vanilla extract, ndizi mbivu na maziwa, halafu endelea kuchanganya.
Weka unga wa ngano, baking soda, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 30 mpaka 35, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.
Leave a Review