Jarida la Mapishi

Keki ya tangawizi na limao

Keki ya tangawizi na limao | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    Dakika 35
  • Kupika
    Dakika 40
  • Walaji
    10

Keki ya tangawizi na limao, ni keki tamu na laini ambayo hupikwa kwa kutumia viungo kama vile tangawizi, limao iliyo kamuliwa, pamoja na maganda ya limao yaliyo kunwa. Keki hii yafaa kula pamoja na kikombe chai au kama kifungua kinywa wakati wa asubuhi. Pia waweza kula keki hii kama kitafunio cha kawaida wakati wowote ule. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya tangawizi na limao.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, unga wa ngano, baking soda, baking powder, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri.

    Step2

    Chukua bakuli nyingine ndogo. Weka ndani ya hiyo bakuli, siagi pamoja na sukari, kisha changanya vizuri. Weka mayai, limao iliyo kamuliwa, maganda ya limao, tangawizi na sour cream, halafu endelea kuchanganya.

    Step3

    Chukua mchanganyiko wa bakuli ndogo ya pili, na umimine kwenye mchanganyiko wa bakuli la kwanza, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.

    Step4

    Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.

    Step5

    Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 35 mpaka 40, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step6

    Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.