-
MaandaliziDakika 20
-
KupikaDakika 40
-
Walaji10
Keki ya vanilla, ni keki tamu na rahisi kupika, iliyo sheheni ladha ya vanilla. Keki hii yaweza kuliwa kama kitindamlo katika hafla ama sherehe ya aina yoyote ile, iwe sherehe ya kuzaliwa au harusi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika keki hii ya vanilla.
Ingredients
Directions
Chukua bakuli kubwa. Weka ndani ya hilo bakuli, siagi, sukari, pamoja na vanilla extract, kisha changanya vizuri.
Weka viini vya mayai 6 na ute wa mayai 2, halafu endelea kuchanganya.
Weka unga wa ngano, baking powder, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri kwa kutumia, mashine ya kuchanganyia (mixer), hadi utakapo ona mchanganyiko huo umechanganyika vyema na kuwa laini.
Chukua sufuria la kuoka keki (cake pan) lenye ukubwa wa nchi 9, na upake siagi. Chukua bakuli lenye mchanganyiko ulio changanya na mashine ya kuchanganyia, na umimine mchanganyiko huo kwenye sufuria la kuoka keki.
Washa jiko la kuoka, na uweke joto la nyuzi 175° C, kisha acha jiko lipate moto. Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka keki ndani ya hilo jiko, na uoke kwa muda wa dakika 30 mpaka 35, au hadi utakapo ona keki imeiva na kuwa na rangi ya kahawia.
Keki ikisha iva, iondoe kwenye jiko la kuoka, kisha iweke pembeni ili ipoe, ikiwa bado ndani ya sufuria la kuoka keki. Keki ikishapoa, unaweza kuitoa ndani ya sufuria la kuoka keki, na kuikata kwa ajili ya kula.
Leave a Review