Jarida la Mapishi

Kuku wa binzari nyembamba na pilipili hoho

Kuku wa binzari nyembamba na pilipili hoho | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 15
  • Walaji
    4

Kuku wa binzari nyembamba na pilipili hoho, ni kitoweo kitamu ambacho hupikwa kwa kutumia nyama ya kuku, pilipili hoho, binzari nyembamba pamoja na viungo vingine. Kitoweo hiki chafaa kula kwenye sherehe za aina mbalimbali. Pia waweza kula kitoweo hiki pamoja na mkate. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika kitoweo hiki cha kuku wa binzari nyembamba na pilipili hoho.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, vipande vya nyama ya kuku, tangawizi, vitunguu swaumu, white vinegar, pilipili manga, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona vipande vyote vya nyama ya kuku vimeenea vyema viungo. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 4 mpaka saa 24.

    Step2

    Chukua kikaango cha ukubwa wa wastani chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, binzari nyembamba pamoja na mchanganyiko wa kuku ulio uweka kwenye friji, kisha pika mchanganyiko huo huku ukivigeuza vipande vya nyama ya kuku mara kwa mara kwa muda wa dakika 7, au hadi utakapo ona vipande vyote vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step3

    Mimina mtindi taratibu huku ukikoroga. Weka vitunguu maji pamoja na pilipili hoho, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona mchuzi umekauka na nyama imeiva.

    Step4

    Weka majani ya giligilani pamoja na garam masala, halafu pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 1, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.