Jarida la Mapishi

Kuku wa kuchoma

Kuku wa kuchoma | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 35
  • Walaji
    4

Kuku wa kuchoma, ni kitoweo kitamu na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kuchanganya nyama ya kuku, viungo, mtindi, limao, pamoja na cream, kisha baadae kuchoma kwenye jiko la kuchomea nyama. Kitoweo hiki chafaa kula pamoja na wali, viazi, mkate au saladi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika kitoweo hiki cha kuku wa kuchoma.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua kuku pamoja na kisu chenye ncha kali, halafu chanja mara 3 kwenye kila kifua cha kuku, na mara 2 kwenye kila paja la kuku, kisha weka kuku kwenye bakuli kubwa.

    Step2

    Chukua kontena dogo. Weka ndani ya hilo kontena, limao pamoja na chumvi, halafu changanya vizuri, kisha paka vizuri mchanganyiko huu kwenye upande wa nje pamoja na upande wa ndani wa kuku. Hakikisha sehemu zote ulizozichanja zimepata mchanganyiko huu. Funika vizuri bakuli hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 2. Baada ya saa 2, ondoa bakuli hilo kwenye friji na uliweke pembeni.

    Step3

    Chukua kontena jingine dogo. Weka ndani ya hilo kontena, mtindi, heavy cream, mafuta ya kupikia, tangawizi, vitunguu swaumu, garam masala, majani ya uwatu, pamoja na binzari nyembamba, halafu changanya vizuri, kisha paka vizuri mchanganyiko huu kwenye upande wa nje pamoja na upande wa ndani wa kuku. Funika vizuri bakuli hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 8 mpaka saa 24.

    Step4

    Washa jiko la kuchomea nyama, kisha acha jiko lipate moto. Weka kuku juu ya hilo jiko, kisha choma huku ukigeuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 20 mpaka 30, au hadi utakapo ona kuku ameiva.

    Step5

    Paka siagi kwenye upande wa nje pamoja na upande wa ndani wa kuku, halafu endelea kuchoma huku ukigeuza mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5 zaidi, kisha ondoa kuku kwenye jiko la kuchomea na uweke kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Conclusion

    Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.