-
Maandalizi-
-
KupikaSaa 1
-
Walaji4
Kuku wa kuoka, ni kitoweo ambacho hupikwa kwa kuchanganya nyama ya kuku, viungo, pamoja na mtindi, kisha baadae kuoka kwenye jiko la kuokea (oven). Kitoweo hiki chafaa kula pamoja na viazi mviringo, mboga, viazi vitamu au saladi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika kitoweo hiki cha kuku wa kuoka.
Ingredients
Directions
Chukua kuku pamoja na kisu chenye ncha kali, kisha chanja mara 3 kwenye kila kifua cha kuku, na mara 2 kwenye kila paja la kuku.
Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, mtindi, mafuta ya kupikia, majani ya giligilani, tangawizi, vitunguu swaumu, pilipili manga, binzari nyembamba, mbegu za shamari, mbegu za giligilani, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri.
Weka kuku, kisha paka vizuri mchanganyiko huo kwenye upande wa nje pamoja na upande wa ndani wa kuku. Hakikisha sehemu zote ulizozichanja zimepata mchanganyiko huu. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 2 mpaka saa 24.
Washa jiko la kuoka (oven), na uweke joto la nyuzi 205° C, kisha acha jiko lipate moto.
Chukua sinia la kuokea. Weka kuku kwenye hilo sinia kwa kumgeuza juu-chini, kisha mimina juu ya huyo kuku, mchanganyiko wa viungo uliobaki kwenye kontena.
Nyunyizia juu ya huyo kuku, karafuu, mdalasini, pamoja na majani ya minti, kisha funika vizuri kuku huyo kwa kutumia aluminium foil.
Weka sinia lenye kuku ndani ya jiko la kuoka, kisha oka kwa muda wa dakika 40, au hadi utakapo ona upande wa juu wa kuku huyo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Punguza moto na uweke joto la nyuzi 190° C. Geuza kuku huyo kwa kumuweka chini-juu, kisha endelea kuoka kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona na upande wa pili wa kuku huyo umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa sinia lenye kuku kwenye jiko la kuoka na uweke pembeni, kisha acha kuku atulie kwa muda dakika 5, kabla ya kula.
Conclusion
Kabla ya kutumia mtindi huo, hakikisha unaupiga piga vizuri ukiwa kwenye bakuli kwa kutumia kijiko kama unavyo yapiga piga mayai unapotaka kuyakaanga, hadi utakapo ona mtindi umekuwa laini na hauna mabonge mabonge.
Leave a Review