Jarida la Mapishi

Kuku wa pilipili

  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 40
  • Walaji
    4

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka tangawizi kwenye hilo sufuria, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, au hadi utakapo ona imebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step2

    Weka vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona vimeiva.

    Step3

    Weka vitunguu swaumu, paprika, pamoja na vipande vya nyama ya kuku, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5.

    Step4

    Weka majani ya giligilani, white vinegar, maji, chumvi, pamoja na pilipili manga, halafu koroga vizuri, kisha weka moto mkubwa na uache ichemke.

    Step5

    Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto wa wastani, halafu acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona maji yamekauka na vipande vya nyama ya kuku vimeiva, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.