Jarida la Mapishi

Kuku wa ukwaju

Kuku wa ukwaju | Jarida la Mapishi
  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 30
  • Walaji
    4

Kuku wa ukwaju, ni kitoweo kitamu na rahisi kupika chenye ladha ya mchanganyiko wa utamu na uchachu, ambacho hupikwa kwa kutumia, nyama ya kuku, sukari, white vinegar, ukwaju, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Chakuka hiki chafaa sana kula pamoja na wali au tambi hasa katika msimu wa sikukuu. Fuata hatua zifuatazo,ili ujifinze jinsi ya kupika kuku wa ukwaju.

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mdalasini, iliki, binzari nyembamba, pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 10, au hadi utakapo ona vitunguu maji vimeiva.

    Step2

    Weka tangawizi pamoja na vitunguu swaumu, kisha koroga vizuri.

    Step3

    Weka vipande vya nyama ya kuku, mbegu za giligilani, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukikoroga na kuvigeuza vipande vya nyama ya kuku mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona vipande hivyo vya nyama ya kuku vimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.

    Step4

    Weka Tamarind Paste, white vinegar pamoja na sukari, halafu pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 8 mpaka 10, au hadi utakapo ona vipande vya nyama ya kuku vimeiva na kuwa laini, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.