-
Maandalizi-
-
Kupika-
-
Walaji2
Lemonade ya strawberry, ni kinywaji rahisi kutengeneza, cha kuburudisha na chenye rangi nzuri ya pinki. Kinywaji hiki hutengenezwa kwa kusaga pamoja matunda halisi ya strawberry, limao, maji, pamoja na sukari. Kinywaji hiki chafaa sana kunywa katika msimu wa kiangazi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza lemonade hii ya strawberry.
Ingredients
Directions
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, limao, apple, matunda ya strawberry, maji, pamoja na sukari, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Chukua chujio, kisha chuja lemonade hiyo vizuri.
Mimina lemonade kwenye chombo safi, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi, kabla ya kunywa.
Conclusion
Unaweza kuongeza maji zaidi, endapo utaona maji yaliyomo katika lemonade hii ni kidogo.
Leave a Review