-
Maandalizi-
-
Kupika-
-
Walaji2
Lemonade ya tikiti, ni kinywaji kitamu, rahisi kutengeneza na cha kuburudisha, ambacho hutengenezwa kwa kusaga pamoja tikiti, limao, apple pamoja na maji. Kinywaji hiki chafaa kunywa katika msimu wa kiangazi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza lemonade hii ya tikiti.
Ingredients
Directions
Step1
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, malimao, apple, tikiti, maji, pamoja na sukari, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Step2
Chukua chujio, kisha chuja lemonade hiyo vizuri.
Step3
Mimina lemonade kwenye chombo safi, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi, kabla ya kunywa.
Conclusion
Unaweza kuongeza maji zaidi, endapo utaona maji yaliyomo katika lemonade hii ni kidogo.
Leave a Review