-
Maandalizi-
-
Kupika-
-
Walaji2
Lemonade ya tikiti na strawberry, chenye rangi nzuri ya pinki na ladha nzuri ya kupendeza, ambacho hutengenezwa kwa kutumia matunda ya strawberry, tikiti, malimao, apple, na maji. Unaweza kuongeza matunda ya strawberry kwenye lemonade hii, endapo unataka ladha ya strawberry itawale zaidi. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kutengeneza lemonade hii ya tikiti na strawberry.
Ingredients
Directions
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, malimao, apple, tikiti, matunda ya strawberry, maji, pamoja na sukari, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.
Chukua chujio, kisha chuja lemonade hiyo vizuri.
Mimina lemonade kwenye chombo safi, kisha iweke kwenye friji ili ipate baridi, kabla ya kunywa.
Conclusion
Unaweza kuongeza maji zaidi, endapo utaona maji yaliyomo katika lemonade hii ni kidogo.
Leave a Review