-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 35
-
Walaji4
Maboga ya kusaga, ni chakula kizuri na chenye afya, ambacho hupikwa kwa kutumia maboga yaliyo sagwa, vitunguu maji, pamoja viungo vya aina mbalimbali. Chakula hiki chafaa kula chenyewe kama kilivyo, au waweza kula pamoja na wali au chapati. Fuata hatua zifutazo ili ujifunze jinsi ya kupika maboga haya ya kusaga.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa lenye mafuta ya kupikia na uliweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hilo sufuria, mbegu za shamari, mbegu za uwatu, black seeds, pamoja na vitunguu maji, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 6, au hadi utakapo ona vitunguu vimeiva.
Weka tangawizi, kisha koroga vizuri.
Weka maboga, kisha kaanga huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7.
Weka mbegu za giligilani, binzari ya manjano, pamoja na chumvi, kisha koroga vizuri.
Ongeza moto na uweke moto mkubwa. Mimina maji halafu koroga vizuri, kisha funika sufuria na uache ichemke kwa muda wa dakika 2.
Punguza moto na uweke moto mdogo, kisha acha iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona maboga yameiva na kuwa laini.
Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, mchanganyiko wa maboga ulio upika, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review