-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 40
-
Walaji4
Magimbi ya kukaanga, ni chakula kitamu na rahisi kupika, ambacho hupikwa kwa kukaanga magimbi yaliyo chemshwa pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Magimbi haya yafaa kula pamoja na chapati au mkate. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika magimbi haya ya kukaanga.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria magimbi pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona yameiva.
Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na magimbi peke yake, kisha acha yapoe.
Menya maganda ya magimbi hayo, kisha yakate katika vipande vidogo vidogo.
Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka nusu ya magimbi kwenye hicho kikaango, kisha kaanga huku ukitikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona upande wa chini wa magimbi hayo umebadilika rangi na kiwa na rangi ya kahawia.
Geuza magimbi upande wa pili, kisha kaanga huku ukitikisa kikaango mara kwa mara kwa muda wa dakika 5, au hadi utakapo ona na upande huo wa pili umebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia.
Nyunyizia mbegu za kisibiti, mbegu za giligilani, binzari nyembamba, binzari ya manjano, mango powder, pamoja na chumvi, kisha kaanga huku ukitikisa kikaango na kuyageuza magimbi mara kwa mara kwa muda wa dakika 2.
Weka majani ya giligilani, halafu kaanga huku ukitikisa kikaango na kuyageuza magimbi mara kwa mara kwa muda wa dakika 2, au hadi utakapo ona majani ya giligilani yamenyauka, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review