-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 50
-
Walaji4
Magimbi ya kuoka, ni chakula chenye ladha nzuri, ambacho hupikwa kwa kutumia magimbi yaliyo chemshwa, limao, pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika magimbi haya ya kuoka.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria magimbi pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona yameiva.
Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na magimbi peke yake, kisha acha yapoe.
Menya maganda ya magimbi hayo, kisha yakate katika vipande vidogo vidogo.
Chukua sinia la kuokea. Weka kwenye hilo sinia, magimbi uliyo yachemsha, mafuta ya kupikia, limao, tangawizi, majani ya giligilani, mbegu za kisibiti, pamoja na chumvi, kisha changanya vizuri.
Washa jiko la kuoka na uweke joto la nyuzi 220° C, kisha acha jiko lipate moto. Weka sinia la kuokea lenye mchanganyiko wa magimbi ndani ya hilo jiko, kisha oka huku ukiyageuza magimbi mara kwa mara kwa muda wa dakika 20 mpaka 30, au hadi utakapo ona yamebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa magimbi hayo kwenye jiko la kuoka na uyaweke pembeni kwenye chombo safi.
Nyunyizia Chaat Masala, kisha changanya vizuri, tayari kwa kula.
Leave a Review