-
Maandalizi-
-
KupikaDakika 45
-
Walaji4
Magimbi yenye nyanya, ni chakula kitamu na chenye ladha nzuri, ambacho hupikwa kwa kutumia magimbi yaliyo chemshwa, nyanya pamoja na viungo vya aina mbalimbali. Fuata hatua zifuatazo, ili ujifunze jinsi ya kupika magimbi haya yenye nyanya.
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria magimbi pamoja na maji, kisha chemsha kwenye jiko lenye moto wa wastani kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona yameiva.
Epua na umwage maji yote yaliyomo kwenye sufuria na kubakiwa na magimbi peke yake, kisha acha yapoe.
Menya maganda ya magimbi hivyo, kisha yakate katika vipande vidogo vidogo.
Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto wa wastani, kisha acha mafuta yapate moto. Weka kwenye hicho kikaango, mbegu za kisibiti, binzari nyembamba, tangawizi, magimbi uliyo yachemsha, pamoja na chumvi, kisha kaanga kwa muda wa dakika 10 huku ukiyageuza magimbi mara 1 au 2, au hadi utakapo ona magimbi yamebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa magimbi hayo kwenye kikaango na uyaweke pembeni kwenye kontena.
Weka kwenye kikaango hicho hicho, nyanya, majani ya giligilani, pamoja na vitunguu swaumu, kisha pika mchanganyiko huo huku ukikoroga mara kwa mara kwa muda wa dakika 5 mpaka 7, au hadi utakapo ona mchuzi umekuwa mzito.
Weka magimbi uliyo yakaanga, kisha pika mchanganyiko huo huku ukiyageuza magimbi mara kwa mara kwa muda wa dakika 3 mpaka 5, au hadi utakapo ona magimbi hayo yamechanganyika vyema pamoja na mchanganyiko wa nyanya.
Nyunyizia Chaat Masala halafu koroga vizuri, kisha epua na upakue kwenye chombo safi, tayari kwa kula.
Leave a Review