Upatikanaji na utumiaji wa ‘jaridalamapishi.co.tz’ ndani na nje ya Tanzania, unawezeshwa na kitengo cha kibiashara cha Hildegard Studios, kwa masharti yafuatayo:
- Kwa kutumia jaridalamapishi.co.tz unakubaliana na kanuni hizi, ambazo zinaanza kutumika mara tu unapoanza kuingia jaridalamapishi.co.tz. Endapo haukubaliani na yote tafadhali usiingie, kutumia na/au kuchangia jaridalamapishi.co.tz.
- Jarida la Mapishi inaweza kubadilisha masharti haya mara kwa mara kwa hiyo ziangalie mara kwa mara. Utumiaji wako wa jaridalamapishi.co.tz utachukuliwa kuwa kukubaliana na masharti yaliyoongezwa au kubadilishwa. Endapo haukubaliani, unatakiwa kuacha kutumia tovuti hii.
Utumiaji wa jaridalamapishi.co.tz
Unakubaliana kutumia jaridalamapishi.co.tz kwa shughuli zinazokubalika kisheria, na vyovyote vile isizuie haki, kukataza mtu yoyote kutumia na kufaidi jaridalamapishi.co.tz.
Mambo yanayo katazwa ni pamoja na unyanyasaji au kusababisha tabu au usumbufu kwa mtu yoyote, kusambaza maudhui yenye matusi au kuvuruga mtiririko wa kawaida ndani ya jaridalamapishi.co.tz.
Haki ya mali akili
Haki miliki zote, nembo za biashara, haki za usanifu, hateza na haki nyingine za mali akili (zilizosajiliwa na ambazo hazijasaliwa) kwenye maudhui ya jaridalamapishi.co.tz na maudhui yote (ikiwa ni pamoja na programu) zilizoko kwenye tovuti zitaendelea kuwa mali ya Jarida la Mapishi.
Hauruhusiwi kunakili, kufyatua upya, kuchapisha upya, kukongoroa, kupangua, kubadilisha kihandisi, kupakua, kutuma, kutangaza, kurusha, au kutoa kwa umma, au vinginevyo kutumia maudhui ya jaridalamapishi.co.tz kwa njia yoyote isipokuwa kwa matumizi yako binafsi na isiwe matumizi ya kibiashara.
Pia unakubali kutokukabilina, kubadilisha au kutengeneza kazi nyingine kutokana na maelezo yoyote ya jaridalamapishi.co.tz isipokuwa tu kwa matumizi yako binafsi yasiyo ya kibiashara. Matumizi mengine yoyote ya maelezo ya jaridalamapishi.co.tz yanahitaji idhini rasmi ya Jarida la Mapishi kimaandishi.
Majina, picha na nembo zinazo itambulisha Jarida la Mapishi, Hildegard Studios au pande nyingine na bidhaa zao na huduma zinalindwa na hakimiliki, haki ya kubuni, na alama za Jarida la Mapishi, Hildegard Studios na/au pande nyingine. Hakuna sehemu ya masharti haya itakayochukuliwa kama ni kutoa leseni yoyote au haki ya kutumia alama yoyote ya kibishara, haki ya kubuni au haki miliki ya Jarida la Mapishi, Hildegard Studios au upande mwingine wowote ule.
Hakimiliki
Haki miliki zote, alama za biashara, haki za kubuni na haki nyingine zote za kazi za ubunifu (zilizosajiliwa au kutosajiliwa) ndani na katika jaridalamapishi.co.tz na maelezo yote (ikijumuisha matumizi yote) yaliyowekwa katika tovuti vitabakia kuwa chini ya Hildegard Studios. Huruhusiwi kunakili, kutoa nakala, kuchapisha upya, kupangua, kuunda upya, kupakua, kutuma, kutangaza, kusambaza, kuwezesha kupatikana kwa umma au vinginevyo kutumia maelezo ya jaridalamapishi.co.tz kwa namna ambayo ni nje ya matumizi yako binafsi, yasiyolenga kibiashara. Pia unakubali kutokukabili na, kubadilisha au kutengeneza kazi nyingine kutokana na maelezo yoyote ya jaridalamapishi.co.tz isipokuwa tu kwa matumizi yako binafsi yasiyo ya kibiashara. Matumizi mengine yoyote ya maelezo ya jaridalamapishi.co.tz yanahitaji idhini rasmi ya Hildegard Studios kimaandishi.
Majina, picha na nembo zinaitambulisha Jarida la Mapishi, Hildegard Studios au pande nyingine na bidhaa zao na huduma zinalindwa na hakimiliki, haki ya kubuni, na alama za Jarida la Mapishi, Hildegard Studios na/au pande nyingine. Hakuna sehemu ya masharti haya itakayochukuliwa kama ni kutoa leseni yoyote au haki ya kutumia alama yoyote ya kibishara, haki ya kubuni au haki miliki ya Jarida la Mapishi, Hildegard Studios au upande mwingine wowote ule.
Ili kushiriki na kutoa mchango katika sehemu zilizochaguliwa za kijamii katika jaridalamapishi.co.tz (ikiwemo ubao wa ujumbe) huenda ukahitajika kuingiza taarifa binafsi. Maelezo yoyote yale ya kibinafsi yanayotolewa kwa jaridalamapishi.co.tz yatachukuliwa, kuhifadhiwa na kutumiwa kulingana na sera ya faragha ya Jarida la Mapishi.
Kanuni za jumuiya
Unakubali kushiriki katika jumuiya zilizopendekezwa za jaridalamapishi.co.tz kulinga na Kanuni za Jumuiya za Jarida la Mapishi zilizo orodhesha hapa chini:
(i). Kuhusu michango yako: • Michango ni lazima iwe ya kiistaarbu na yenye mvuto. • Mwenendo wa usumbufu, kuchukiza au matusi hauruhusiwi: michango lazima iwe ya kujenga na yenye heshima, isiwe na lengo baya au iliyotolewa kwa kusudi la kusababisha kero. • Mchango ulio kinyume cha sheria hauruhusiwi: michango iliyo kinyume cha sheria, usumbufu, udhalilishaji, unyanyasaji, vitisho, kudhuru, matusi, yenye lengo la kimapenzi, ubaguzi wa rangi au vinginevyo haikubaliki. • Uwe mvumilivu: Watumiaji wa rika zote na uwezo huenda wakaweza kushiriki katika jumuiya husika za jaridalamapishi.co.tz. • Michango iliyo nje ya mada au yenye lengo la kudhuru hairuhusiwi. • Hairuhusiwi matangazo au kujitangaza.
Michango iliyo katika lugha nyingine zaidi ya (lugha yako mfano Kiswahili) huenda ikaondolewa.
Hairuhusiwi kujiigiza kuwa mtu mwingine. • Hairuhusiwi majina yasiyokubalika. (mfano yenye kuchukiza)
(ii). Usalama: Tunashauri kuwa kamwe usitoe maelezo binasi kuhusu wewe mwenyewe au mtu mwingine yeyote yule moja kwa moja kwa umma katika jumuiya yoyote ile ya Jarida la Mapishi.
(iii). Mahitaji ya kisheria: • Usiwasilishe au kubadilidhana mchango wowote wa kudhalilisha au ulio kinyume cha sheria kwa namna yoyote ile katika jumuiya za jaridalamapishi.co.tz.
Maelezo ya mchango kwa jaridalamapishi.co.tz jumuiya yenye lengo la kufanya au kutangaza kitendo kilicho kinyume cha sheria inapigwa marufuku vikali.
(iv). Iwapo una umri chini ya miaka 16:
Tafadhali pata idhini ya mzazi au mlezi kabla hujashiriki katika jumuiya zozote zile za jaridalamapishi.co.tz.
Kamwe usitoe maelezo binafsi kuhusu wewe mwenyewe au mtu mwingine yeyote yule (kwa mfano shule, namba ya simu, jina lako kamili, anwani ya nyumbani au anwani ya barua pepe).
Kukana na Kupunguza Wigo wa Uwajibikaji
Sehemu kubwa ya mchango unaotumwa katika jumuiya za jaridalamapishi.co.tz inafanywa na umma. Maoni yanayotolewa ni ya kwao na isipokuwa pale imeelezwa vinginevyo, maoni hayo si ya Jarida la Mapishi au Hildegard Studios. Jarida la Mapishi na Hildegard Studios haihusiki na mchango wa maelezo yoyote yaliyotumwa na umma katika jaridalamapishi.co.tz. Viunganishi vyovyote vile kwa upande mwingine wa tovuti kutoka jaridalamapishi.co.tz haimaanishi tovuti hiyo imeidhinishwa na Jarida la Mapishi au Hildegard Studios na matumizi yoyote ya tovuti hiyo ni kwa athari yako mwenyewe.
Michango ya jaridalamapishi.co.tz, ikiwemo maelezo, majina, picha, logo, zinazohusiana na Jarida la Mapishi na/au Hildegard Studios, ni bidhaa na huduma (au kwa upande mwingine wa bidhaa na huduma), inatolewa “KAMA NI” na katika “KAMA INAVYOPATIKANA” kimsingi. Katika kiwango kinachoruhusiwa kisheria, Jarida la Mapishi inaondoa uwakilishi na udhamini wote (iwe imeelezewa au kumaanishwa kisheria), ikiwemo udhamini unaomaanishwa katika kiwango cha kuridhisha, kufaa kwa dhumuni maalum, isiyokiuka, inayokubaliana, ulinzi na usahihi. Jarida la Mapishi haihakikishii muda maalum, umalizikaji au utendendaji kazi wa tovuti au maelezo yoyote yale. Wakati tunajaribu kuhakikisha kuwa maelezo yote yanayotolewa na Jarida la Mapishi ni sahihi wakati wa uchapishaji, hakuna lawama yoyote inayopokelewa na au kwa niaba ya Jarida la Mapishi kwa makosa yoyote yale, kusahauliwa au maelezo yasiyo sahihi katika tovuti.
Hakuna kitu chochote katika masharti haya kinacho iondolea Jarida la Mapishi uwajibikaji au lawama juu ya kifo au maumivu yanayo sababishwa na uzembe wake uliothibitibitika. Kwa mujibu wa sentensi iliyo tangulia, Jarida la Mapishi na/au Hildegard Studios haitawajibika kwa upotevu wowote ule au uharibifu ufuatao (iwe uharibifu huo au upotevu ulitabirika, kujulikana au vinginevyo): (a) kupotea kwa data; (b) kupotea kwa mapato au faida iliyotarajiwa; (c) kupotea kwa biashara; (d) kupotea kwa nafasi; (e) kupotea kwa nia njema au kuathirika kwa hadhi; (f) upotevu ulizoziathiri pande nyingine; au (g) matokeo au athari yoyote ile isiyo ya moja kwa moja maalum au uharibifu unaotokana na matumizi ya jaridalamapishi.co.tz bila kujali kuchukuliwa hatua.
Jarida la Mapishi na Hildegard Studios haitoi hakikisho kuwa ufanyaji kazi unaopatikana katika jaridalamapishi.co.tz hautaingiliwa au kutokuwa na makosa, kwamba makosa yatarekebishwa, au kwamba jaridalamapishi.co.tz au seva inayowezesha upatikani wake haiwezi kuwa na virusi. Unakubali kuwa ni wajibu wako kutumia utaratibu unaohitajika na kukagua virusi (ikiwemo kipinga virusi na ukaguzi mwingine wa kiusalama) kutosheleza mahitaji yako maalum kwa usahihi wa data zinazoingia na kutoka.
Kushindwa au kuchelewa kwa Jarida la Mapishi kutekeleza au kusimamia yoyote kati ya masharti haya haiiondolei Jarida la Mapishi haki hiyo.
Masharti haya yatasimamiwa na kutafsiriwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania ambazo ndizo pekee zitatumika kutatua mgogoro wowote wa kisheria.
Wiji
Kwa kutumia kuonyesha maudhui ya Jarida la Mapishi (“Maudhui ya Jarida la Mapishi”) kwenye kompyuta yako unakubaliana na masharti yaliyo ainishwa hapo chini.
Masharti ya Wiji
Waranti na Uwajibikaji
2.1 Wiji za Jarida la Mapishi na Maudhui ya Jarida la Mapishi zinaundwa kwa msingi wa “kama zilivyo” na “kama zinavyopatikana” na unatumia Wiji za Jarida la Mapishi na kuangalia Maudhui ya Jarida la Mapishi kwa utashi na madhila yako.
2.2 Jarida la Mapishi imechukua tahadhari kuhakikisha kuwa Wiji za Jarida la Mapishi na Maudhui ya Jarida la Mapishi kuepusha upungufu, makosa, virusi au hitilafu, hata hivyo Jarida la Mapishi haisemi kila kitu kitafanya kazi bila matatizo.
2.3 Kadiri inavyo ruhusiwa kisheria, Jarida la Mapishi haitoi hakikisho la aina yoyote (lidhaniwalo, lazima au vinginevyo) kuhusiana na Wiji ya Jarida la Mapishi, Maudhui ya Jarida la Mapishi au tovuti ya Jarida la Mapishi na Jarida la Mapishi haitahusika kwa hasara yoyote au uharibifu utakaotokana au kuhusishwa na Wiji ya Jarida la Mapishi au Maudhui ya Jarida la Mapishi.
2.4 Unashauriwa kuchukua tahadhari zote kulinda kompyuta yako isiambukizwe virusi.
2.5 Jarida la Mapishi inaweza kubadilisha Maudhui ya Jarida la Mapishi kwa utashi wake na inaweza kuzuia matumizi ya Wiji ya Jarida la Mapishi endapo utakiuka Sheria hizi za Matumizi ya Mwisho.
Jumla
3.1 Masharti haya ya Matumizi ya Mwisho yatatafsiriwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania na mashauri yatasimamiwa tu na Mahakama za Tanzania.
Ujumla
Iwapo masharti yoyote katika haya yanaonekana kuwa ni kinyume cha sheria, batili au vinginevyo hayawezekani kutekelezeka kutokana na sababu za kisheria katika nchi au jimbo lolote lile ambako masharti haya yamelengwa kufanya kazi, basi kwa kiwango na ndani ya uwezo wa kisheria ambako masharti hayo ni kinyume na sheria, batili au hayatekelezeki, yatafutwa kutoka katika masharti haya na masharti yaliyobaki yataendelea kuwepo na kutumika.
Kushindwa au kuchelewa kwa Jarida la Mapishi kufanyia kazi au kutekeleza haki yoyote ile katika masharti haya haiondolei Jarida la Mapishi haki ya kutekeleza haki hiyo.