-
Maandalizi-
-
KupikaSaa 2
-
Walaji4
Ingredients
Directions
Chukua sufuria kubwa. Weka kwenye hilo sufuria, karafuu, mdalasini, majani ya mbei, iliki, mbegu za shamari, pilipili manga, kungumanga, nyama za mbavu, maziwa, pamoja na ½ kijiko cha chai cha chumvi, halafu koroga vizuri, kisha weka ichemke kwenye jiko lenye moto mkubwa.
Ukiona imeanza kuchemka, punguza moto na uweke moto mdogo, kisha funika sufuria na uache iendelee kuchemka kwa muda wa dakika 20 mpaka 30, au hadi utakapo ona mbavu zimeiva na maziwa yote kwenye sufuria yamekauka.
Zima jiko, kisha acha ipoe walau kwa muda wa saa 1.
Chukua kontena la ukubwa wa wastani. Weka ndani ya hilo kontena, unga wa dengu, unga wa mchele, ute wa yai, tangawizi, ½ kijiko cha cha chi cha chumvi iliyobaki, pamoja na maji, kisha piga piga vizuri mchanganyiko huo, hadi utakapo ona umechanganyika vizuri na kuwa laini.
Chukua kikaango kikubwa chenye mafuta ya kupikia na ukiweke kwenye jiko lenye moto mkubwa, kisha acha mafuta yapate moto.
Mimina Yogurt Cheese kwenye sufuria lenye mbavu, halafu changanya vizuri hadi utakapo ona mbavu zote zimeenea vyema Yogurt Cheese, kisha chovya mbavu hizo kwenye kontena lenye mchanganyiko wa viungo.
Weka kwenye hicho kikaango, mbavu ambazo zinatosha na kuenea kwenye kikaango, kisha kaanga huku ukizigeuza mara kwa mara, hadi utakapo ona zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa mbavu hizo kwenye kikaango na uziweke pembeni kwenye chombo safi chenye paper towel, ili zikauke mafuta, kabla ya kula. Rudia hatua hii kwa mbavu zilizobaki.
Leave a Review