Jarida la Mapishi

Mbavu za kuoka

  • Maandalizi
    -
  • Kupika
    Dakika 20
  • Walaji
    4

Ingredients

    Directions

    Step1

    Chukua mashine ya kusaga (blender). Weka kwenye hiyo mashine ya kusaga, korosho, iliki, mbegu za uwatu, pamoja na mbegu za binzari nyembamba, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri. Ondoa mchanganyiko huo kwenye mashine ya kusaga na uweke pembeni kwenye kontena.

    Step2

    Weka kwenye hiyo hiyo mashine ya kusaga, vitunguu swaumu, tangawizi, pamoja na majani ya minti, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo umesagika vizuri na kuwa laini.

    Step3

    Weka Yogurt Cheese, limao, mafuta ya kupikia, mchanganyiko wa korosho ulio usaga, garam masala, pamoja na chumvi, kisha saga hadi utakapo ona mchanganyiko huo wote umechanganyika vizuri.

    Step4

    Chukua kontena kubwa. Weka ndani ya hilo kontena, nyama za mbavu, pamoja na mchanganyiko ulio usaga, kisha changanya vizuri hadi utakapo ona mbavu zote vimeenea vyema viungo. Funika vizuri kontena hilo, kisha liweke kwenye friji kwa muda wa saa 12 mpaka saa 24.

    Step5

    Washa jiko la kuoka na uweke joto la nyuzi 260° C, kisha acha jiko lipate moto.

    Step6

    Chukua sinia la kuokea. Weka mchanganyiko wa nyama za mbavu kwenye hilo sinia, halafu weka sinia hilo ndani ya jiko la kuoka, kisha oka kwa muda wa dakika 20, au hadi utakapo ona mbavu zimebadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia. Ondoa sinia hilo lenye mbavu kwenye jiko la kuoka na uliweke pembeni, kisha kata mbavu hizo, tayari kwa kula.

    Unaweza Pia Kusoma Hizi

    Leave a Review

    Your email address will not be published. Required fields are marked *


    The reCAPTCHA verification period has expired. Please reload the page.